Hii ni blogu ya habari mbalimbali za dunia,zikiwemo za kushangaza,kuchekesha,na hata kuelimisha.

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.
[6] [ALL] [slider-top] [READ THIS]

Sababu za Ajabu za kukufanya ufanye mauaji


     

1
Kijana aliyemuua mama yake kisa tiketi za Avril Lavigne

The son who killed his mother over Avril Lavigne tickets
  Mnamo mwaka 2012, mwanaume aliyekua na umri wa miaka 39 na mkazi wa Chicago nchini Marekani alihukumiwa kifungo cha miaka 40 jela kwa mauaji ya mama yake mzazi aliyofanya mwaka 2008. Inasemekana kuwa alifanya kitendo hicho baada ya mamake kukataa kumnunulia tiketi za yeye kuweza kuhudhuria tamasha la mwanamuziki Avril Lavigne.

2.Mvulana aliyemuua dada yake kwa kugombania "remote control"

The boy who killed his sister for the possession of a remote control
Mwaka 2011, mvulana wa miaka 13 alisemekana kumuua dada yake wakati wakigombania "remote control". Mvulana huyo alimfyatulia risasi dada yake usoni na kusababisha kifo chake,hiyo ilitokea huko Siberia.


3.Wapenzi waliouawa kwa kumu-unfriend mtu Facebook.

The couple who was killed for unfriending someone on Facebook
Mnamo mwaka 2012, Billy Payne Jr.,36, na mpenzi wake, Billie Jean Hayworth, 23, walimfuta urafiki Jenelle Potter, 30, katika Facebook. Jenelle alihuzunika, lakini si kama alivyohuzunika baba yake, Marvin "Buddy" Potter. alikasirika sana,kiasi kwamba akaenda kuwaua wapenzi hao,ambao wameacha mtoto mmoja wa kiume.

4.Jamaa aliyeua polisi kisa nafasi ya kuegesha gari

The man who killed an off-duty officer over a parking space
  Mnamo 2010, jamaa mwenye umri wa miaka 25 na mkazi wa baltimore nchini marekani alifikishwa mahakamani kwa mauaji ya afisa wa polisi baada ya kumpiga na kipande cha tofali kichwani,hiyo ilitokea wakati wakigombania nafasi ya kuegesha gari.

5.Jamaa aliyeua kisa muziki wa Rap

The man sentenced to life for killing teen over 'rap music'
Mnamo mwezi Oktoba mwaka 2014, Michael Dunn alihukumiwa maisha jela baada ya kumuua kijana mwenye asili ya Afrika wa umri wa miaka 17 sababu ikiwa kijana huyo kufungulia muziki wa rap kwa sauti ya juu ambayo ilimkera jamaa huyu.